KAMDOMO TU KIUNO KIMEPOA POOH EPISODE 4


 Si ndio kuangalia picha sasa kwenye simu😂. Wote wawili walikuwa wameweka mikono. Lilikuwa ni pozi zuri kupita maelezo.


"Itapendeza kama tutapiga picha bila kuweka mikono " Ariana alishauri.

Yasin hakuwa tayari kujiangalia, acha avunge kama hajasikia 😅

Ariana alimpotezea, ilifika mahali ndege ikashuka kwenye kituo kwa ajili ya kula.

Yasin ni kumfuata tu Ariana kwa nyuma.

"Mbona unanifuata shida nini?"

"Mimi ni mvivu kula pekee yangu, itapendeza kama tutakaa wote meza moja usiwe na shaka nitalipia bili ya chakula "

"Oooh sawa " Ariana aliongea kisha akakaa kwenye kiti.

Yasin ni mtaalamu sana wa kuchagua menu nzuri.

Kwa pamoja walianza kula, Ariana alikuwa anakula kama anafukuzwa hivi. Ilifika mahali akajishtukia kwa sababu alikuwa anaelekea kumaliza sahani yake ilihali Yasin ndio kwanza alikuwa kama anaanza.

"Isije kuwa kashiba minofu na damu za binadamu ...." Ariana aliongea na moyo wake kisha akaidaka sahani ya Yasin.

Utafunaji wa Ariana ulimfurahisha Yasin, alijikuta akimrekodi kijanja.

Ariana ndio kushtuka kuwa anarekodiwa.

"Kitu gani hicho unafanya naomba ufute hiyo video mara moja"

"Ni vile nilivutiwa tu na namna unavyo tafuna hii hapa nafuta " Yasin aliongea kisha akaihamishia Google drive ndipo akaifuta.

Muda kula uliisha, kwa pamoja walirudi kwenye ndege.

Ariana si alikuwa ameshiba kupita kiasi kazi aliyokuwa nayo ni kukoroma tu. Mishuzi ilikuwa ikimpita kama yote.

Alilalala hivi akalala vile mwisho wa siku alidondokea begani kwa Yasin Kijana Mwarabu.

Domo lake lilikaa wazi likawa linapenyeza tu udenda. Yasin alivumilia kuogeshwa na maji ya mdomoni.

Hatimaye ndege ilitua uwanja wa ndege, Ariana ndio kushtuka. Macho yalimtoka baada ya kuona kalowanisha shati ya watu. Alivunga kama hajafanya chochote.

"Nadhani tutatengana hapa, kwa kuwa nina mawasiliano yako nitakutafuta. Naomba utafutike please, nikimaanisha upokee simu " Yasin aliongea.

"Usijali nitapokea simu "

Wakiwa hapa gari maalumu ilikuja kumchukua Yasin. Alifunguliwa mlango kwa heshima zote. Yote haya yakiwa yanaendelea Ariana alishuhudia na ndipo alipata kuelewa kuwa huyu mtu si level zake. Ingawa na yeye ni wakishua lakini huyu ni moto wa kuotea mbali.

Alishtuka katika fikira zake baada ya manyunyu ya mvua kumdondokea. Akiwa anawaza atapata wapi usafiri ilikuja tax ya kishua ikasimama karibu yake.

"Mr. Yasin kaniagiza nikupeleke sehemu uliyokusudia kwenda " Dreva mwenye asili kizungu aliongea kwa Kiingereza.

"Mr. Yasin "

Dreva hakutaka kuongea sana alimuonesha picha ya Yasin.

Ariana hakuweza kuleta ubishi, alimsihi Dreva ampeleke kwenye hoteli yoyote ile yenye mandhari mazuri.

Basi baada ya kupata chumba, alishika simu yake akampigia Eva video call.



"Ulikuwa sahihi my dear, huyu mtu si jini 😅 sina uhakika kama alizaliwa. Hawa ni wale watu wanaogizwa tu kutoka Dubai, China au India."

"Nikiwa katika maombi nilikuona ukiwa na Mwanaume mzuri sana mkiitana wanandoa nina uhakika wakati wa wewe kufurahi unakuja " Eva aliongea.

Ariana alimkatia simu, baada ya kupokea kichambo kitakatifu kutoka kwa ex wake Mike hataki kabisa kusikia neno mahusiano.

Alivua nguo zake zote akasalia na chupi tu. Ndio tabia zake hizi kulala hivi hasa akiwa pekee yake.

Ghafla kengele ilisikika mlangoni kwake. Alichukua taulo akataka kwenda kufungua mlango lakini kabla hajafanya hivyo aliwasha TV ndogo iliyokuwa ukutani ili amuone Mgeni. Aliachia tabasamu baada ya kumuona Mhudumu.

Ile anafungua mlango alishtuka kumuona Yasin akiwa pembeni ya Mhudumu.

Ni kitu gani kimemleta hapa Yasin......

ITAENDELEA.......

Post a Comment

0 Comments